• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa 6 wa mfumo wa mawasiliano kati ya vyama tawala vya China na Japan wafanyika nchini Japan

  (GMT+08:00) 2017-08-09 18:10:43

  Mkutano wa 6 wa mfumo wa mawasiliano kati ya vyama tawala vya China na Japan ulioitishwa na chama cha kikomunisti cha China, na vyama cha uhuru na demokrasia na New Komeito vya Japan umefanyika kuanzia jumanne wiki hii na kumalizika leo nchini Japan.

  Ujumbe a China uliongozwa na mkurugenzi wa idara ya mawasiliano na nchi za nje ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China Bw. Song Tao. Katika hotuba yake, Bw. Song amesema ikiwa ni miaka 45 tangu uhusiano wa kibalozi kati ya China na Japan uwe kawaida, vyama tawala vya nchi hizo mbili vimefanya mkutano wa mfumo wa mawasiliano vikilenga kutekeleza makubaliano muhimu ya viongozi wa nchi hizo mbili, kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili uendelee kwa mweleko sahihi.

  Amezitaka pande hizo mbili zitekeleze kanuni na nia ya nyaraka 4 za siasa za China na Japan, na kutatua masuala nyeti kuhusu historia na Taiwan kwa njia mwafaka, kulinda msingi wa kisiasa wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili, kuhimiza mawasiliano katika sekta mbalimbali, kujadili ushirikiano kwenye msingi wa Ukanda Moja na Njia Moja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako