• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu 19 wafariki katika tetemeko la ardhi nchini China

  (GMT+08:00) 2017-08-09 18:16:53
  Idadi ya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea mkoa wa Sichuan jana imefikia 19 huku wengine 247 wakijeruhiwa.

  Kati ya watu waliofariki kutokana na tetemeko hilo lenye ukubwa wa 7.0 kwenye kipimo cha Richter ni watalii waliokuwa kwenye eneo maarufu la utalii la Jiuzhaigou, ambalo ni maarufu kwa maporomoko ya maji.

  Rais Xi Jinping wa China na waziri mkuu Li Keqiang wametoa wito wa juhudi zaidi kufanyika katika kazi za uokoaji na kutoa misaada.

  Habari nyingine zinasema, watu 32 wamejeruhiwa kutokana na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.6 kutokea katika kaunti ya Jinghe iliyoko mkoani Xinjiang, kaskazini magharibi mwa China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako