• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Askari sita wajeruhiwa baada ya kugongwa na gari nchini Ufaransa

  (GMT+08:00) 2017-08-09 19:00:40

  Askari sita wamejeruhiwa, wawili kati yao vibaya, baada ya gari moja kugonga kikosi cha askari kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa Ufaransa, Paris, leo asubuhi, na kisha kukimbia.

  Meya wa eneo la Levallois-Perret, Patrick Balkany amelieleza tukio hilo kuwa ni uvamizi. Amesema gari aina ya BMW lililoegeshwa kwenye uchochoro mmoja liliwagonga askari hao walipokuwa wanatoka kwenye kambi yao wakielekea kwenye doria.

  Uchunguzi wa tukio hilo umeanza, na dereva pamoja na gari lililohusika wanatafutwa na polisi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako