• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwezakeji wa China katika nchi za nje utafikia dola trilioni 1.5 za kimarekani katika miaka 10 ijayo

    (GMT+08:00) 2017-08-09 19:00:42

    Ripoti iliyotolewa na shirika la sheria la Kimataifa Linklaters LLP imesema, huenda uwekezaji wa China katika nchi za nje utafikia dola trilioni 1.5 za kimarekani katika miaka 10 ijayo, wakati sera za China zitaimarisha uwekezaji katika nchi za nje.

    Ripoti hiyo imekadiria kuwa, uwekezaji huo unatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 70 katika miaka 10 ijayo. Pia ripoti hiyo imesema, uwekezaji na manunuzi ya mashirika katika nchi za nje kutoka China utaendelea kuwa nguvu kubwa katika miaka kadhaa ijayo kufuatia sera na mipango ya muda mrefu ya China ikiwemo "Made in China 2025" na pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako