• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wajenzi watimiza thamani yao kwa kuchangia upandaji wa msitu wa Saihanba

  (GMT+08:00) 2017-08-09 20:05:11
  Msitu wa Saihanba ulioko umbali wa kilomita 200 kutoka Beijing, ulikuwa jangwa kubwa miaka 55 iliyopita, lakini sasa umebadilika na kuwa msitu wenye eneo kubwa zaidi duniani uliopandwa na watu. Je, ni nani walichangia mabadiliko hayo?

  Bw. Yu Shitao alianza kufanya kazi katika msitu wa Saihanba baada ya kuhitimu shahada ya kwanza katika chuo kikuu. Tofautia na yeye, mkewe Fu Lihua alifanya kazi kwa miaka mitatu katika kampuni moja ya China baada kumaliza masomo yake ya shahada ya pili katika Chuo cha sayansi ya mambo ya misitu. Aliacha kazi mjini Beijing kwenda kwenye msitu huo kuishi na mumewe. Akikumbusha siku za mwanzoni walipoanza kuishi katika msitu huo, Fu Lihua alisema hata sasa bado hajazoeza kabisa maisha ya huko. Anasema: "Ni tofauti na kuishi mjini Beijing ambako kuna burudani nyingi usiku, na niliweza kula pamoja na wenzangu baada ya kazi na kutembelea maduka, kwa kawaida nililala baada ya saa tano usiku. Lakini hapa msituni baada ya kazi hakuna burudani yoyote, hali ambayo inanifanya nijisikie upweke."

  Fu Lihua anakabiliana na upweke, ikilinganishwa naye, wenzake walikuwa walikumbwa na mazingira magumu zaidi katika miaka kadhaa iliyopita. Msitu wa Saihanba uko umbali mkubwa kutoka mjini, na hali ya miundo mbinu iko nyuma sana. Hata hadi kufikia mwaka 2000, mazingira ya msitu huo yalikuwa mabaya sana. Mkuu wa Kituo cha kulinda usalama cha msitu huo Bw. Guo Zhifeng anasema: "Nakumbuka vizuri sana, nilifika kwenye msitu huo Julai 9, 2000, na kutumwa milimani tarehe 10. Wakati ule ulikuwa msimu wa mvua, ambapo magari, vyakula hata mboga zilishindwa kufikishwa kwenye eneo la msitu. Wakati mvua zikinyesha kwa siku 6 hadi 7 mfululizo, kulikuwa hakuna mboga, niliweza kula wali tu. Wakati ule nilijiuliza ni kwanini upashanaji wa habari ulikuwa na urahisi sana katika sehemu nyingine, lakini hapa msituni bado hali iko nyuma namna hii."

  Kutokana na kukabiliana na mazingira magumu na maisha ya upweke, baadhi ya watu waliamua kuondoka, lakini wengine wanaendelea kuishi hapa. Guo Zhifeng ni mmoja kati ya watu hao. Katika msitu huo uliopandwa na watu, maafa ya wadudu ni tishio kubwa zaidi. Guo Zhifeng na wenzake walibuni njia za kutabiri maafa ya wadudu, na kiwango cha usahihi kinazidi asilimia 90, tena wanapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya dawa za kikemikali ili kupunguza athari mbaya kwa mazingira. Guo Zhifeng anasema: "Tulipofanya sensa ya viumbe kati ya mwaka 2014 hadi 2016, tuligundua aina moja ya mdudu anayeitwa Snakefly ambaye anaishi katika sehemu yenye mazingira mazuri, endapo mazingira yakichafuliwa anaondoka. Hivyo tulifurahi sana kumwona, kwani uwepo wake ni dalili ya mazingira mazuri."

  Licha ya kukabiliana na changamoto mbalimbali maishani katika msitu, Fu Lihua kamwe hakuwa na majuto hata kidogo kuchagua kuishi hapa. Anasema: "Naridhika na kazi yangu, kwani hii ni kozi yangu niliyoisomea chuo kikuu. Nafurahia kufanya utafiti wa sayansi kwa kutumia masomo yangu."

  Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2016, eneo la miti lilifikia hekta elfu 74.7 kwenye msitu wa Sailinba, kiasi hicho kinafikia asilimia 80 ya eneo la jumla la misitu hiyo, na kuufanya msitu wa Saihanba kuwa msitu wenye eneo kubwa zaidi duniani lililopandwa na watu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako