• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kiongozi wa upinzani kenya apinga matokeo ya uchaguzi mkuu

  (GMT+08:00) 2017-08-09 20:31:27

  Hali ya utulivu inashudiwa nchini kenya baada ya uchaguzi mkuu kukamilika nchini humo hapo jana.

  Hata hivyo kiongozi wa upinzani nchini humio Raila Odinga amedai kwamba kumekuwa na udukuzi wa mitambo ya tume ya uchaguzi na kwamba matokeo yanayoonyesha kwamba rais Uhuru Kenyatta ameshinda sio sahihi.

  Mwandishi wetu Tom wanjala ametutumia ripoti ifuatayo.

  Kulingana na matokeo kwenye mtandao wa tume huru ya uchaguzi nchini Kenya, rais uhuru Kenyatta anaongoza kwa zaidi ya kura milioni 7.8 ikiwa ni asilimia 54.3.

  Kiongozi wa upinzani naye anayeongoza muuungano wa NASA Raila Odinga ana kura milioni 6.5 sawa na asilimia 44.7.

  Hayo hata hivyo ni matokeo ya hadi saa nane hivi wakati tukienda hewani kutoka hapa katika kituo cha kujumuisha kura cha Kitaifa kilichoko ukumbi wa Bomas.

  Lakini huku wakenya wakiwa na hisia na maoni mbalimbali kuhusu matokeo hayo ya kura ya Agosti 8, sasa kiongozi wa upinzani Raila Odinga amedai kwamba mitambo ya tume huru ya Uchaguzi ilidukuliwa na hivyo kuathiri matokeo ya uchaguzi kumfaidi Rais Uhuru Kenyatta.

  "Nataka kuwaeleza wakenya kwamba tumeweza kufichua wizi ya kura ambayo ilifanyika jana, kwenye tume ya Uchaguzi. Kuna njama ambayo ilikuwa imepangwa na watu wakaingia kwenye mitambo ya IEBC. Watu hao wanajulikana na wengine wako kwenye ukumbi wa Bomas."

  Mapema leo Raila akiandamana na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka walikuwa na mkutano na waandishi wa habari ambako pia wamehusisha kudukuliwa na mitambo ya IEBC na kuuwawa kwa aliyekuwa meneja wa teknolojia wa IEBC Chris Msando.

  Lakini madai hayo yapingwa vikali na upande wa chama tawala cha Jubilee ukisema hakuna wizi au udukuzi uliofanyika na wanachofanya NASA ni kutafuta vijisababu tu vya kukataa matokeo.Huyu hapa ni katibu mkuu wa chama cha Jubilee Rapahel Tuju.

  "Kwa Mara nyingine tena tungependa kuangalia kwa makini taakwimu na idadi ya kura tulizo nazo, haya matokeo hayajana utata na hajatokea tu lakini ni matokeo ya kweli kulingana na sisi, na huwezi kudai kwamba matokeo ya urais yako sawa lakini yale ya magavana na wabunge huna tatizo nayo. Unafaa kukubali matokeo."

  Lakini Raila Odinga Waziri mkuu wa zamani nchini humo amesema sasa bado hawataenda mahakamni kwanza kupinga matokeo hayo huku wakiwataka wafuasi wao kuwa watulivu.

  "Tunawaambia wakenya wawe watulivu na tutaendelea kuchunguza na kuwaambia hatua tutakayochukua"

  Mwenye kiti wa tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka Wafula Chebukati anasema kila upande haki ya kuwalisha malalamishi yao na tume hiyo itachunguza madai yoyote yale.Hata hivyo ameondoa hofu kwamba kuna matatizo na matokeo ya sasa hata bila fomu nambari 34 ambayo bado haujatolewa.

  "Nataka kusema matokeo ambayo tulitangaza kwenye vituo vya kupigia kura yako sawa"

  Hadi sasa kuhusu usalama ni kwamba hakuna matukio yoyote yale ya ghasia yalioshudiwa kote nchini na baadhi ya wakenya wameanza kurejea biashara na shughuli zao za kila siku.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako