• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Biashara zafungwa Kenya kufuatia uchaguzi

  (GMT+08:00) 2017-08-09 21:00:28

  Wafanyabiashara nchini Kenya wakadiria hasara baada ya wengi kufunga biashara zao kutokana na uchaguzi Mkuu uloandaliwa jana,ambao bado matokeo kamili ya uchaguzi huo hayajakamilika.

  Wafanyabiashara hao hususan wenye maduka ya vipuri vya magari,maduka ya jumla,usafiri wa magari ya umma na maduka mengineyo mijini bado wamefunga biashara zao.

  Miji mikuu ya Kenya kama vile Nairobi na Mombasa imesalia kuwa mahame huku kukiwa hakuna pilkapilka zozote za biashara.

  Wachunguzi wanaona kuwa uchaguzi, hususan nchini Kenya, una kawaida ya kuleta hali ya wasiwasi ambayo inaathiri wateja, na hivyo kufanya maendeleo yoyote kuwa katika hali ya hatihati.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako