• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Usafirishaji wa bidhaa za Kenya kuingia Tanzania wapungua kwa asilimia 34

  (GMT+08:00) 2017-08-09 21:02:25

  Usafirishaji wa bidhaa za Kenya kuingia Tanzania umepungua kwa asilimia 34 katika kipindi cha miezi mitano iliyopita,ikiwa ni kiashiria cha matokeo hasi ya vizuizi vinavyowekwa kwa biashara.

  Biashara imeporomoka kwa Ksh4.35bn (Tsh87bn) hadi Ksh8.2bn (Tsh164bn) mpaka kufikia Mei mwaka huu,ikilinganishwa na Ksh12.55bn (Tsh251bn) zilizorekodiwa katika kipindi kama hicho mwaka jana.

  Kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Takwimu ya Kenya (KNBS) ,usafirishaji wa bidhaa kwenda Uganda umeendelea kukua na kuimarisha nafasi ya nchi hiyo katika bidhaa zinazozalishwa viwandani.

  Kwa upande mwingine ,Tanzania imekuwa kwenye mgogoro wa muda mrefu wa kufikia masoko ya Kenya,mgogoro ambao uliongezeka zaidi mwezi Mei baada ya Tume ya Udhibiti wa Nishati ya Kenya kupiga marufuku kuingizwa kwa gesi nchini humo kupitia mpaka wa Namanga kwa kile walichodai ni sababu za kura.

  Hata hivyo Tanzania ilijibu mapigo kwa kuzuia uingizwaji wa maziwa na sigara kutoka Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako