• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kilimo kuchangia pakubwa pato la Taifa Tanzania

  (GMT+08:00) 2017-08-09 21:04:20

  Serikali ya Tanzania imesema kuwa licha ya sekta ya madini kutajwa kuwa kinara katika uchangiaji wa Pato la Taifa, sekta ya kilimo inapaswa kushika namba moja kutokana na kuhusisha watu wengi kwenye uzalishaji wake.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene alipokuwa akitoa hotuba ya kufunga maonesho ya sherehe za Wakulima (Nanenane) kwenye Uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya kwa niaba ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu.

  Simbachawene alisema kilimo ni namba moja katika uchangiaji wa Pato la Taifa kutokana na kuhusisha watu wengi na kutoa ajira ya moja kwa moja kuanzia ngazi ya uzalishaji, uongezaji wa thamani na wakati wa kuuza bidhaa zake.

  Alisema pia sekta ya kilimo ndiyo msingi na shabaha ya serikali katika kuepukana na njaa kwani kupitia sekta ya kilimo inayohusisha idara ya mifugo, uvuvi, nyuki, misitu na kilimo, kunafanya kuondokana na umasikini ili kufikia uchumi wa viwanda.

  Aliongeza kuwa mwaka huu kuna ziada ya chakula kwa asilimia 20 huku mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ikiwa ndiyo kinara kwa uzalishaji kutokana na fursa ya hali ya hewa nzuri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako