• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda-Wafanyabiashara wa Uganda wasita kupunguza bidhaa kupitia bandari ya Mombasa kutokana na uchaguzi

  (GMT+08:00) 2017-08-09 21:04:41

  Wafanyabiashara wa Uganda wamepunguza uagizaji wa bidhaa zao kupitia bandari ya Mombasa kutokana na uchaguzi Mkuu nchini Kenya.

  Mashirika mbalimbali ya habari yaliripoti kuwa sarafu ya Uganda haikubadilika wakati Kenya ikifanya uchaguzi,jambo lililosababisha waagizaji wengi kutotumia bandari ya Mombasa,na kupunguza hitaji la sarafu ya dola ya marekani.

  Punguzo la hitaji la dola ya marekani inaoonyesha kuwa wafanyabiashara wamesita kuagiza bidhaa kupitia bandari ya Mombasa kwa kuhofia labda huenda kukwa na ghasia za uchaguzi.

  Licha ya kuwa bandari ya Mombasa ndiyo inayopendwa sana na wafanyabiashara wa Uganda,ghasia za uchaguzi wa mwaka 2007/2008 zilizusha mjadala iwapo wafanyabiashara wa Uganda watahamia bandari ya Dar es Salaam.

  Hata hivyo kufikia sasa uchaguzi Mkuu wa Kenya umetekelezwa kwa amani,na hakuna visa vyovyote vya ghasia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako