• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri wa ulinzi wa Marekani atoa onyo kwa Korea Kaskazini kusimamisha utafiti wa silaha za nyuklia

  (GMT+08:00) 2017-08-10 10:13:04

  Waziri wa ulinzi wa Marekani James Mattis amesema, Marekani na nchi washirika zimeonesha uwezo wa kuzuia shambulizi la aina yoyote. Korea Kaskazini inapaswa kusimamisha mpango wake wa utafiti wa silaha za nyuklia.

  Kwenye taarifa yake Bw. Mattis amesema, rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un anapaswa kuzingatia kauli ya pamoja ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na taarifa za nchi mbalimbali ambazo zinaona Korea Kaskazini inatishia usalama na utulivu wa dunia.

  Bw. Mattis pia amesema, Marekani na nchi washirika zina nguvu ya kujilinda na kushambulia. Kitendo chochote cha Korea Kaskazini cha kufanya mashindano ya silaha hakitafua dafu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako