• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Ulaya umesema hatua mwafaka zimeendelea kuiletea Ulaya ufufukaji wa uchumi

  (GMT+08:00) 2017-08-10 10:16:09

  Kamati ya Umoja wa Ulaya imetoa taarifa kuwa Umoja wa Ulaya umechukua hatua mwafaka katika miaka kumi iliyopita katika kuzuia kuenea kwa msukosuko wa uchumi wa Ulaya, na kuchangia katika ukuaji wa uchumi katika miaka mitano iliyopita.

  Taarifa hiyo imesema hatua mwafaka zimeleta ukuaji huo, idadi ya watu wasio na ajira imepungua na kuwa chini kabisa tangu mwaka 2008, nguvu ya sekta ya benki imeongezeka, na uwekezaji kutoka nje umeongezeka. Lakini athari ya msukosuko wa uchumi bado ipo, juhudi za kuhimiza kuongeza nafasi za ajira na kuhakikisha usawa kwenye jamii zinatakiwa kufanyika.

  Naibu mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Ulaya Bw Valdis Dombrovskis amesema Umoja wa Ulaya unatakiwa kuboresha umoja wa kifedha uliopo, kuhimiza mageuzi ya kiuchumi, kujenga uchumi shirikishi na kudumisha maendeleo endelevu katika mfumo wa fedha za umma.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako