• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kinadada wa Kenya wafuzu fainali za mbio za kuruka maji na viunzi

  (GMT+08:00) 2017-08-10 10:41:46
  Mwanariadha wa Kenya ambaye ni bingwa wa dunia katika mbio za mita 3,000 kuruka maji na viunzi Hyvin Kiyeng aliwaongoza wenzake Purity Kirui, Cellphine Chespol na Beatrice Chepkoech katika kufuzu fainali za mbio za wanawake za mita 3,000 kuruka maji na viunzi katika mashindano ya dunia yanayoendelea London.

  Kiyeng, bingwa wa mashindano ya jumuiya ya madola katika mbio hizo purity Kirui, na bingwa wa dunia katika mbio za mita 3000 za chipukizi Cellphine Chespol na Beatrice Chepkoech walifuzu kwa fainali itakayoandaliwa ijumaa usiku.

  Kiyeng na Kirui waliongoza kwa wakati mmoja lakini ni Gesa Felicitas Krause kutoka Ujerumani ambaye alishinda nusu fainali ya kwanza. Kiyeng, aliyeshinda medali ya fedha kwenye mashindano ya Olimpiki ya Rio mwaka uliopita, alimaliza wa pili akifuatiwa na Kirui.

  Hata hivyo, Chepkoech na Chepsol walishinda nusu fainali zao bila kutoa jasho na kuwezesha Kenya kuwa na nyota wanne katika fainali kuamua nani atatwaa medali siku ya Ijumaa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako