• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shija na Selasela wasisimua kinyanganyiro TFF

  (GMT+08:00) 2017-08-10 10:42:06
  Mwaniaji wa urais katika shirikisho la kandanda nchini Tanzania TFF katika uchaguzi unaosubiriwa kwa hamu Shija Richard, alizindua kampeini yake siku ya Jumatano akiahidi kurejesha uadilifu katika shirikisho hilo pamoja na kukuza talanta katika mchezo wa soka kote nchini.

  Shija alisema hayo baada ya kamati ya uchaguzi ya shirikisho hilo kumuidhinisha kuwania kiti hicho pamoja na wagombea wengine wa viti mbalimbali katika uchaguzi huo utakaofanyika wikendi hii jijini Dodoma.

  Kulingana na manifesto yake, Shija ana mambo kadhaa ambazo amezipa kipaumbele iwapo atachaguliwa kwenye wadhifa huo wa juu kwenye shirikisho hilo. Shija amesema mambo mengine ni ya kutekeleza kwa kipindi kifupi ilihali mengine ameyaratibisha yafanyike kwa kipindi kirefu ili kuwezesha kandanda nchini Tanzania kuingia hatua nyingine kwani kulingana naye maendeleo hayapatikani kwa siku moja.

  Shija, anayekabiliwa na upinzani kutoka wawaniaji tano kwa wadhifa wa rais, analenga kutambua na kukuza vipaji nchini pamoja na kutoa mafunzo kabambe kwa makocha, wauguzi wa spoti, marefa na wasimamizi wa soka kote nchini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako