• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Timu ya wanabaiskeli ya Rwanda yasaka taji Marekani.

  (GMT+08:00) 2017-08-10 10:42:27
  Timu ya wanabaiskeli ya Rwanda maarufu kama Team Rwanda itaanza harakati zake za kushinda taji la mwaka huu la Colorado Classic baadaye Alhamis. Mashindano hayo yenye hatua 4 kwenye kitengo cha 2.HC UCI, wenye umbali wa kilomita 503, itaendelea hadi Agosti 13 Marekani.

  Wakishiriki katika mashindano hayo ya hali ya juu kwa mara ya kwanza kabisa, wanabaiskeli wa Rwanda wanatazamia kuanza vyema mashindano hayo dhidi ya waendeshaji baiskeli maarufu duniani na vilabu vinavyoshiriki mashindano hayo kama vile BMC Racing Team, kati ya wengine.

  Jumla ya wanabaiskeli 90 wa kiume watashiriki mashindano ya leo ya hatua ya kwanza ambayo ni refu na ngumu sana yenye umbali wa kilomita 150.4.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako