• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Makocha wa Cranes, Amavubi wanatazamia mchuano wa CHAN

  (GMT+08:00) 2017-08-10 10:42:49
  Moses Basena na Antoine Hey wanafahamu fika kwamba kushiriki kwa timu zao katika mashindano ya kombe la bara afrika CHAN yatakayoandaliwa mwakani nchini Kenya huenda ukaamuliwa katika mchuano baina ya timu hizo utakaochezwa siku ya jumamosi uwanjani St Mary's, Kitende.

  Rwanda ilijiandaa kwa muchuano huu kwa kushinda timu kutoka Sudan bao 2-1 katika mechi ya kirafiki siku ya jumatatu ilihali Uganda ilitoka sare bao 2-2 na klabu kutoka Tanzania ya Azam FC, siku moja baadaye.

  Uganda itaalika Rwanda kwa mchuano huo wikendi hii ikifahamu kwamba ushindi nyumbani itawapa nafasi nzuri vijana wa Cranes kumaliza vyema wiki moja baadye jijini kampala kwa mechi ya marudiano, na kujikatia tikiti kuingia mashindano ya CHAN.

  Kocha wa Uganda Basena anasema lengo lake ni kuhakikisha timu yake imeshinda mechi ya Jumamosi. Hata hivyo kocha Antoine Hey wa Rwanda anatarajia timu yake itapangua mipango ya Uganda na kumaliza vyema mbele ya mashibiki wake timu hizo zitakaporudiana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako