• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Roger Federer apaa Montreal

  (GMT+08:00) 2017-08-10 10:43:10

  Roger Federer alianza vyema maandalizi yake ya mashindano ya US Open katika mashindano ya ATP Montreal Masters siku ya Jumatano, kwa kumshinda mchezaji wa Canada Peter Polansky kwa seti mtawalia na kufuzu kwa raundi ya tatu.

  Nyota huyo kutoka Uswizi, aliyesherehekea miaka 36 tangu kuzaliwa kwake siku ya Jumanne, alimlemea mwenzake anayeorodheshwa nambari 116 duniani na kushinda 6-2, 6-1 katika dakika 53.

  Federer anapaa baada ya mwaka uliojaa mafanikio kwake ambapo tayari ameshinda mataji ya Australian Open na Wimbledon.

  Hapo jana, Federer alidhihirisha kwamba ana uwezo wa kutwaa na kuongeza taji la US Open baada ya mchezo maridadi uliomwacha Polansky bila majibu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako