• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Paul Kagame aendelea na urais wa Rwanda baada ya kupata kura nyingi kabisa

  (GMT+08:00) 2017-08-10 10:57:43

  Tume ya uchaguzi ya Rwanda imetangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi mkuu mjini Kigali, na kusema mgombea wa Chama cha RPF, Bw Paul Kagame ameshinda kwenye uchaguzi huo na ataendelea kuwa rais wa Rwanda.

  Takwimu zilizotolewa na tume ya uchaguzi zimeonyesha kuwa watu milioni 6.9 walishiriki kwenye upigaji kura, kiasi ambacho ni asilimia 98 ya idadi ya jumla ya wapiga kura waliojiandikishwa. Bw Kagame amepata zaidi ya kura milioni 6.6, sawa na asilimia 98.79 ya kura zote.

  Mgombea huru Bw Philippe Mpayimana amepata nafasi ya pili kwa kupata asilimia 0.73 ya kura, Bw Frank Habinezawa Chama cha Kijani amepata asilimia 0.48 ya kura.

  Paul Kagame mwenye umri wa miaka 59 amepata uungaji mkono kutokana na kuhimiza maafikiano ya kitaifa na kujenga upya taifa baada ya vita, na kuleta utulivu wa kisiasa na maendeleo ya kiuchumi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako