• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa uko tayari kutoa msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi wa China

    (GMT+08:00) 2017-08-10 11:00:08

    Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema, umoja huo uko tayari kutoa msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Sichuan, nchini China.

    Bw. Dujarric ametoa salamu za pole kwa serikali ya China na wananchi wake, na kusema licha ya kuwa serikali ya China ina uzoefu mkubwa wa utafutaji na uokoaji baada ya tetemeko la ardhi, Umoja wa Mataifa umefanya maandalizi ya kutoa msaada kama serikali ya China ikitoa ombi la msaada wa kimataifa.

    Habari zinasema mpaka sasa watu 19 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 200 wamejeruhiwa kwenye tetemeko hilo la ardhi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako