• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zaidi ya watalii 50,000 wahamishwa baada ya tetemeko kutokea kusini magharibi mwa China

  (GMT+08:00) 2017-08-10 16:27:09

  Zaidi ya watalii elfu 50, wakiwemo raia 126 wa kigeni, wamehamishwa baada ya kutokea tetemeko kubwa la ardhi mkoani Sichuan, kusini magharibi mwa China jumanne wiki hii.

  Mamlaka ya mkoa huo imesema, watalii hao wamepelekwa kwenye maeneo salama ikiwemo miji ya Mianyang na Chengdu, na pia zaidi ya wakazi elfu tisa wa huko wamehamishwa.

  Waokoaji waliwapata watu 16 walionaswa kwenye eneo la utalii linalojulikana kama Panda Sea katika wilaya ya Jiuzhaigou, na juhudi za kuwaokoa zinaendelea.

  Wakati huohuo, idadi ya vifo vilivyosababishwa na tetemeko hilo imefikia 20 huku watu wengine 431 wakijeruhiwa, 18 kati yao wakiwa kwenye hali mbaya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako