• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Mataifa wasisitiza ulinzi wa wazawa wa asili

  (GMT+08:00) 2017-08-10 16:27:41

  Umoja wa Mataifa umeadhimisha miaka 10 tangu kupitisha Azimio la Haki za Watu Wazawa kwa kusisitiza haja ya kuondoa ubaguzi, kutengwa, na kukiuka haki zao.

  Taarifa ya pamoja iliyotolewa na mashirika 40 ya Umoja huo na mashirika mengine ya kimataifa kuadhimisha siku hiyo imesema, wakati wazawa wamepata maendeleo makubwa katika kutetea haki zao katika nyanja ya kimataifa na kikanda, bado utekelezaji wa azimio hilo unakwama kutokana na kutengwa na mazingira hatarishi, hususan wazawa wanawake, watoto, vijana, na wale wenye ulemavu.

  Taarifa hiyo imesema, ingawa baadhi ya nchi zimechukua hatua za kikatiba na kisheria kutambua haki za wananchi wazawa na utambulisho wao, bado kutengwa, kubaguliwa, na vurugu dhidi yao vinaendelea kuenea.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako