• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shirika la UnionPay la China lafanya ushirikiano na Benki ya Biashara ya Kenya

  (GMT+08:00) 2017-08-10 18:44:45

  Kampuni tanzu ya shirikisho la kadi za benki la China UnionPay International imetangaza kuwa itafanya ushirikiano wa kina na Benki ya Biashara ya Kenya KCB, kutoa kadi ya kwanza ya UnionPay inayotumia huduma ya kulipa ya QuickPass nchini Kenya, ambayo itainua kiwango cha huduma ya malipo nchini humo.

  Kampuni hiyo imesema, kwa kuwa kadi za UnionPay zinaweza kutumiwa kwenye tovuti rasmi ya shirika la ndege la Kenya, maduka zaidi ya mia moja kwenye mtandao wa Internet yatafungua huduma ya kulipa kupitia kadi za UnionPay kabla ya mwezi Januari mwaka kesho.

  Pia kampuni hiyo imesema, hivi sasa asilimia 90 ya maduka na asilimia 75 ya mashine za ATM zinatumia huduma ya malipo kupitia kadi za UnionPay. KCB imefungua huduma ya kadi za UnionPay katika maduka na mashine za ATM nchini Kenya, Burundi, Rwanda, Tanzania na Uganda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako