• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mtu mmoja auawa katika milipuko ya mabomu mjini Kabul, Afghanistan

  (GMT+08:00) 2017-08-10 18:45:05

  Mtu mmoja ameuawa na wengine saba kujeruhiwa katika milipuko miwili ya mabomu iliyotokea Kabul, mji mkuu wa Afghanistan.

  Habari zinasema, mtu mmoja akiwa kwenye gari lililotegwa bomu alijaribu kushambulia msafara wa magari ya kikosi cha usalama cha taifa, na kulipua bomu hilo baada ya kugunduliwa na askari. Mlipuko huo umesababisha raia watatu kujeruhiwa na mshambuliaji huyo kufa papo hapo. Kundi la Taliban limetangaza kuhusika na shambulizi hilo.

  Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo Bw. Najib Danis amesema, bomu lingine lililotegwa kwenye gari lililipuka jana usiku na kusababisha askari wanne kujeruhiwa.

  Habari nyingine zinasema, wapiganaji wa kundi la Taliban wametwaa tena makao makuu ya wilaya ya Jani Khil mkoani Paktia nchini Afghanistan.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako