• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda:Dawa ghushi za kutibu saratani zagunduliwa Uganda

  (GMT+08:00) 2017-08-10 20:52:26

  Halmashauri ya kitaifa ya dawa za matibabu nchini Uganda imetoa onyo kwa wananchi wa Uganda kuhusiana na kusambaa kwa dawa feki za kutibu saratani.

  Msemaji wa halmashauri hiyo Frederick Ssekyana amesema dawa aina ya Sutent na Avastin zimepatikana katika baadhi ya maduka nchini Uganda.

  Halmashauri hiyo imetoa taarifa rasmi kwa wahudumu wa afya nchini Uganda kufanya uchunguzi wa dawa hizo ili kuzuia wateja kuuziwa dawa hizo.

  Kwa mujibu wa uchunguzi wao,wateja wamekuwa wakiuziwa dawa hizo kwa shilingi milioni 3.

  Utafiti huo unaonyesha kwamba dawa hizo hazitumiki kwa njia yoyote kupunguza makali ya saratani .

  Baadhi wa wafanyibiashara wanaouza dawa hizo wameshtakiwa .

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako