• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda:Shughuli za biashara nchini Kenya zaendelea kudorora

  (GMT+08:00) 2017-08-10 20:54:17

  Shughuli za biashara na uchumi nchini Kenya zimeendelea kusalia chini wakati ambapo wakenya wanasubiri matokeo ya uchaguzi mkuu wa urais.

  Jijini Nairobi mbalo ndio jiji kuu biashara nchini Kenya wafanyibiashara wamefungua maduka na viwanda ila idadi ya wateja imeaslia haba.

  Bidhaa muhimu kama mikate,maziwa,mboga zimekosekana madukani baada ya shuhuli nyingi za uchukuzi kusimamishwa.

  Barabara kuu ya kutoka Mombasa hadi Nairobi inayotumika kusafirisha bidhaa kutoka bandarini hadi nchi jirani za Afrika Mashariki imekua na magari machache tofauti na ilivyo kawaida.

  Rwanda imesema kwamba itasitisha baadhi ya biashara zake na Kenya wiki hii kuhofia hasara inayoweza kutokea kulingana na hali tete ya sasa.

  Kwa sasa Rwanda inatumia Bandar ya Tanzania katika kupitisha bidhaa zao kutoka ulaya.

  Hali hii inajiri baada ya kiongozi wa upinzani ambae ni mgombeaji mkuu wa urais Raila Odinga kutangaza kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako