• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya:Wapangaji walalamikia ada za nyumba

  (GMT+08:00) 2017-08-10 20:54:38

  Wapangaji ama walipaji nyumba za kukodi wamelalamikia ongezeko la bei hizo mwaka huu.

  Hii ni baada ya serikali ya Kenya Kuanzisha utekelezaji wa sheria mpya kukusanya ushuru kupitia kwa malipo ya wafanyikazi walioajriwa,mikopo ya benki za biashara,ushuru wa bidhaa na hata wapangaji.

  Kuanzia mwezi wa Aprili KRA itaweka maajenti wa kukusanya ushuru wa moja kwa moja kutoka kwa wapangaji watakaolipa asilimia 10 kama ushuru.

  Ushuru huu unalipwa tarehe 20 ya kila mwezi na wanaokosa kulipa watapigwa faini ya asilimia 10 pamoja na riba ya asilimia 1.

  Rotich amesema lengo la kutekeleza sheria hii mpya iliofanyiwa marekebisho mwaka 2016 ni kuongezea kipato kwa serikali.

  Ukosefu wa kulipa ada za maji,umeme na mawasiliano aidha utatozwa faini ama ushuru.

  Hata hivyo wafanyikazi walioajiriwa watapewa afueni ndogo ya ushuru, kwa mfano wanaolipwa mshahara wa elfu 40 wataondolewa ushuru wa shilingi 500.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako