• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania:Viwanda kulipa kodi

  (GMT+08:00) 2017-08-10 20:56:43

  Serikali ya Tanzania imesema kuanzia mwaka huu itatangaza kodi ambayo watu wote wenye viwanja nchini, wakiwemo wanaoishi katika makazi yasiyopimwa, wataanza kulipa kodi hiyo ya ardhi kwa kuhakikisha wananchi wote wanaishi katika makazi yaliyorasimishwa.

  Imesema wanaoishi katika makazi yasiyopimwa watatambuliwa kwa kupewa leseni za makazi zitakazokuwa na ukomo, wakitakiwa kuishi kwa muda utakaopangwa na baada ya kipindi hicho kumalizika, watatakiwa maeneo yao yawe yameshapimwa tofauti na hivyo manispaa zitaagizwa kufunga nyumba zao. Aidha, imesema serikali haitojihusisha tena katika kupima maeneo yoyote ya ardhi kuanzia sasa, na badala yake kinachotakiwa ni wananchi wenyewe kuwajibika kwa kuunda kamati za urasimishaji zitakazosaidia maeneo yao kupimwa.

  Kadhalika imesema katika kudhibiti matapeli wa ardhi, na migogoro mbalimbali ya ardhi, inaanzisha mradi mpya utakaoanzia katika Manispaa ya Ubungo na Kinondoni ambao utawezesha kutoa hati za makazi katika njia ya elektroniki. Hata hivyo, imetoa hati 84 za makazi kwa wananchi wa Kata ya Kimara, Mtaa wa Kilungule A Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam na tayari viwanja 4,333 vimeshapimwa, ikiwa ni utekelezwaji wa mpango darasa wa kupima viwanja 6,000 vya kata hiyo na mitaa yake sita.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako