• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa asikitishwa na kufa maji kwa wahamiaji toka Afrika

  (GMT+08:00) 2017-08-11 09:17:11

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Antonio Guterres amesema amesikitishwa na ripoti kuwa watu wanaosafirisha wahamiaji kwa magendo kutoka pembe ya Afrika kwenda Yemen, wamewatosa wahamiaji hao na kusababisha vifo vya wahamiaji zaidi ya 50.

  Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema, mbali na waethiopia na wasomali waliokufa jana, wahamiaji wengine 180 walitoswa baharini, miili ya watu watano imepatikana na watu zaidi ya 50 hawajulikani walipo. Umoja wa mataifa unatoa msaada wa maji, chakula na misaada mingine ya dharura kwa watu waliookolewa.

  Wiki iliyopita umoja wa mataifa ulitoa tahadhari kuhusu vitendo vya wasafirishaji wahamiaji kwa magendo, kuwapa wahamiaji hao ahadi za magendo, na kuwatosa wahamiaji kwenye pwani ya Yemen, ili kukwepa kukamatwa na mamlaka za huko.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako