• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Vikosi vya usalama vya Somalia vyazuia shambulizi mjini Mogadishu.

  (GMT+08:00) 2017-08-11 09:34:16

  Vikosi vya usalama nchini Somalia vimezuia shambulizi la bomu lililotegwa kwenye gari karibu na hoteli moja mjini Mogadishu.

  Msemaji wa wizara ya usalama wa ndani ya Somalia Bw Ahmed Mohamud amesema mabomu hayo yaliyojazwa kwenye gari yakilengwa hoteli hiyo yaliteguliwa bila kuwepo majeruhi yeyote. Amesema vikosi vya usalama vilipata taarifa mapema juu ya uwezekano wa kutokea shambulizi hilo na hatimaye kugundua gari linaloshukiwa.

  Wakati huohuo serikali ya Somalia imetangaza kuwa kiongozi mkuu wa kundi la Al-Shabaab ameuawa kwenye shambulizi la anga. Wizara ya habari imesema kiongozi huyo alikuwa sehemu ya mtandao wa Al-Shabaab unaohusika kupanga na kutekeleza mashambulizi mengi ya mabomu na mauaji mjini Mogadishu ambayo yamesababisha vifo vya raia wasio na hatia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako