• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda yakamilisha kuondoa askari wake kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati

  (GMT+08:00) 2017-08-11 10:24:47

  Jeshi la Uganda limekamilisha kuondoa askari wake 2,500 wanaowasaka waasi wa Kundi la Lord's Resistance Army LRA nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

  Naibu msemaji wa jeshi la ulinzi la umma la Uganda Bw Deo Akiiki amesema kundi la mwisho la askari hao limerudi Uganda Jamatano chini ya uongozi wa kamanda Richard Otto. Kazi ya kuwaondoa askari hao kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati imemalizika, na vifaa vyote vimerudi Uganda jana usiku.

  Ameongeza kuwa vikosi vya Jamhuri ya Afrika ya Kati na Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati vinaendelea kukabiliana na tishio kutoka Kundi la LRA.

  Shirika la madaktari wasio na mipaka MSF limetoa taarifa kwamba mapambano yaliyotokea mjini Batangafo, kaskazini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati yamesababisha vifo vya watu 24 na wengine 17 kujeruhiwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako