• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Benki ya maendeleo ya nchi za BRICS kuanzisha tawi la kwanza la kikanda nchini Afrika Kusini

  (GMT+08:00) 2017-08-11 10:25:09

  Mkuu wa Benki ya maendeleo ya nchi za BRICS Bw Kamath amesema benki hiyo itaanzasha tawi lake la kwanza la kikanda nchini Afrika Kusini tarehe 17 mwezi huu.

  Bw. Kamath amesema kwa mujibu wa mipango ya benki hiyo, theluthi mbili ya miradi ya mkopo ni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu itakayojengwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Mchakato wa maendeleo ya kundi jipya la uchumi umeonyesha umuhimu wa maendeleo endelevu, kuunga mkono ujenzi wa miundombinu ni muhimu kwa nchi wanachama.

  Bw Kamath amesema tawi jipya litakaloanzishwa mjini Johannesburg wiki ijayo ni tawi la kwanza la kikanda la benki hiyo, ambalo litasaidia kuhimiza miradi yake barani Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako