• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Julius Yego akata tikiti fainali ya kurusha mkuki

  (GMT+08:00) 2017-08-11 10:35:30
  Mkenya Julius Yego yuko mbioni kutetea taji lake la dunia katika mashindano ya kurusha mkuki baada ya jaribio la kwanza kurusha mkuki ambapo alifuzu moja kwa moja kwa fainali za wanaume katika mchezo huo utakaoandaliwa siku ya Jumamosi kwenye uwanja wa Olympic jijini London.

  Yego, aliyeingia mashindano hayo akiwa amerusha mkuki kwa rekodi mzuri ya mita 87.97, aliweza kutupa mita 83.57 na kufuzu katika kundi la A ambapo mchezaji anayeongoza dunia kwa sasa Johannes Vetter kutoka Ujerumani anayejivunia kurusha mita 94.44 aliongoza kwa kutimu mita 91.20.

  Yego, ambaye pia ni mshindi wa medali ya fedha katika olimpiki na bingwa wa mashindano jumuia ya madola alifanya jinsi alivyoahidi kwamba atajaribu kufanya vyema katika jaribio lake la kwanza la kurusha mkuki itakayomwezesha kufuzu fainali katika uwanja aliyoandikisha rekodi miaka tano iliyopita.

  Yego, mwenye umri wa miaka 28, aliandikisha historia kuwa Mkenya wa kwanza kushiriki mashindano kando na riadha katika mashindano ya olimpiki jijini London mwaka wa 2012.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako