• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni ya Giunness yaahidi mwamko mpya raga Uganda

  (GMT+08:00) 2017-08-11 10:36:08
  Baada ya kuandikisha matokeo mazuri timu ya raga ya wachezaji 7 kila upande ya Uganda sasa imepata udhamini zaidi kutoka Guinness, ambayo ni mojawapo ya kampuni ya bidhaa ya Uganda Breweries Limited (UBL), ambayo imeahidi kuweka mkataba mpya wa kufadhili timu hiyo kwa miaka mitatu ijayo.

  Meneja wa kampuni hiyo Estella Muzito amesema Guinuess imerejelea majukumu yake ya kufadhili raga kwani wanafiriki ni wakati mzuri wa kuboresha na kuinua viwango vya raga nchini Uganda.

  Kulingana na Muzito, makubaliano ya ufadhili huo unafikia shilingi milioni 200 pesa za Uganda lakini akasema Giunness inatoa shilingi milioni 100 pesa taslimu ilihali nusu yake itatolewa kwa njia ya msaada mbalimbali.

  Mchezo wa raga wa wachezaji 7 kila upande nchini Uganda kwa miaka nyingi umehisi kutopewa kipaumbele kama inavyofanyiwa raga ya wachezaji 15, lakini baada ya kushinda kombe la Afrika "Africa Cup" mwaka uliopita ulifungua ukurasa mpya kwa timu hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako