• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shirikisho la soka Tanzania TFF kuandaa uchaguzi Jumamosi

  (GMT+08:00) 2017-08-11 10:45:31

  KAMATI ya rufani ya uchaguzi wa TFF iliyoketi juzi Jumanne, imewarejesha baadhi ya wagombea waliokuwa wameenguliwa awali wakiwemo wanne waliotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa. Kikao hicho kilichofanyika Ukumbi wa St. Gasper kilifanya uamuzi mgumu.

  Sasa orodha ya mwisho baada ya baadhi ya wagombea kufanikiwa kushinda rufaa zao katika Kamati ya Rufaa za uchaguzi wanaowania urais ni pamoja na Wallace Karia, Imani Madega, Fredrick Mwakalebela, Ally Mayay, Shija Richard na Emmanuel Kimbe.

  Jumla ya rufani zilizowasilishwa mezani kwao ni tano ambazo zilikuwa zinahusu kuanza kampeni mapema na tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa huku rufani nyingine ikiwa ni uzoefu wa kusimamia mpira iliyomhusu Mwenyekiti wa Chama cha soka Singida, Mussa Sima.

  Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Keneth Mwenda alisema baada ya kupitia maelezo na nyaraka zote zilizowasilishwa kamati hiyo ilibaini kuwa warufani wote hawakupewa fursa ya kuhojiwa."

  Kwa chini ya masaa 24 wawaniaji hao hatimaye watakutana kwa debe kuamua ni nani atayechukua hatamu za uongozi katika shirikisho la kandanda Tanzania TFF.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako