• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mradi wa China wa kusaidia vijiji elfu 10 kutazama televisheni za satelaiti wachangia katika kuhimiza maendeleo ya teknolojia za dijitali barani Afrika

  (GMT+08:00) 2017-08-11 10:52:53

  Sherehe ya uzinduzi wa mradi wa majaribio wa televisheni za satelaiti ilifanyika Agosti 10, 2017 katika kijiji cha Hulumi, kitongoji cha Abuja, mji mkuu wa Nigeria, ambapo iliwashirikisha naibu mkurugenzi wa Ofisi ya habari ya baraza la serikali la China Bw. Guo Weimin, mwenyekiti wa kamati ya habari kwenye baraza la juu la bunge la Nigeria Bw. Suleiman Adokwe pamoja na wajumbe wengine kutoka pande hizo mbili.

  Bw. Guo Weimin amesema huu ni mradi muhimu katika mradi wa "kwezesha vijiji elfu 10 barani Afrika kutazama televisheni za satelaiti" uliotangazwa na mwezi Septemba mwaka 2015 na rais Xi Jinping kwenye mkutano wa viongozi wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, na unalenga kuinua kiwango cha maendeleo ya televisheni za dijitali kwa kutumia teknolojia na vifaa vya China, na kuongeza njia za kupata habari kwa wakazi wa huko, ili kuhimiza maelewano na urafiki kati ya watu wa China na nchi za Afrika.

  Meneja mkuu wa Kituo cha televisheni cha taifa la Nigeria Bw. Yakubu Ibn Mohammed amesema, anafurahia kampuni ya Startimes ya China kuzawadia televisheni za dijitali kwa sehemu maskini, hatua ambayo inasaidia serikali ya Nigeria katika kuinua kiwango cha maisha ya wenyeji wa huko.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako