• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wapiganaji 30 wa kundi la Taliban wauawa katika ajali ya mlipuko nchini Afghanistan
   

  (GMT+08:00) 2017-08-11 16:23:53
  Wapiganaji 30 wa kundi la Taliban wameuawa katika mlipuko uliotokea kwa bahati mbaya kwenye mkoa wa Farah, magharibi mwa Afghanistan hapo jana.

  Msemaji wa serikali ya mkoa huo Nasir Mehri amesema, mlipuko huo umetokea kwenye kijiji cha Pewa Pasaw wilaya ya Bala Buluk, kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa mkoa huo Farah, kabla ya wapiganaji hao kujaribu kufanya shambulizi dhidi ya maeneo ya vikosi vya usalama. Amesema wakati wapiganaji hao wakijiandaa kwa shambulizi hilo, moja ya jaketi lililotegwa mabomu lililipuka kabla ya muda, hivyo kusababisha milipuko mfululizo iliyosababisha vifo hivyo na wapiganaji wachache nao kujeruhiwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako