• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zaidi ya watoto laki 5 wanahitaji msaada nchini Libya

  (GMT+08:00) 2017-08-11 16:27:29

  Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema mgogoro unaoendelea na hali mbaya ya uchumi nchini Libya vimewaacha watoto laki 5 wakihitaji msaada wa kibinadamu nchini humo.

  Mkurugenzi wa UNICEF kanda ya Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika Geert Cappelaere amesema, mapigano makali katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo yamezilazimisha familia kukimbia makazi yao. Amesema zaidi ya watoto elfu 80 ni wakimbizi wa ndani na watoto wahamiaji nchini Libya wako kwenye hatari zaidi ya kutumiwa kwa malengo mabaya na kuteswa.

  Tangu mwaka 2011, UNICEF imekuwa ikiongeza msaada wake ili kukabiliana na mahitaji ya watoto nchini Libya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako