• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bei ya vyakula yapanda kufuatia kuathirika kwa sekta ya usafiri

  (GMT+08:00) 2017-08-11 17:59:23

  Bei ya vyakula nchini Kenya imepanda kufuatia kuathirika kwa shughuli za usafiri wakati huu ambapo kila mkenya anasubiri matokeo ya uchaguzi wa urais.Baadhi ya bidhaa mbazo bei inaonekana kupanda ni mahhindi, karoti, maharage, mboga, kitunguu na tomato. Hii imetokana na ukosefu wa usafirishaji wa bidhaa hizi hadi kwa wateja waliotapakaa katika sehemu mbali mbali nchini Kenya.Baadhi ya wasafirishaji walioongea na radio China Kimataifa wamesema wanahofia usalama wao wakati huu ambapo kumekuwa na msukosuko wa kisiasa nchini Kenya.Wafanya biashara wengi wanaomiliki maduka ya vyakula wamesema hifadhi zao zimepungua hali ambayo imepelekea bei kupanda. Kenya ilifanya uchaguzi tarehe nane mwezi huu na hadi kufikia sasa matokeo ya urais hayajatolewa huku vyama vya Jubilee na NASA vikidai kushinda uchaguzi huo. Hata hivyo hali huenda ikarudi ya kawaida baada ya tume ya uchaguzi kuahidi kumtangaza mshindi wa urais leo mchana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako