• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wazalishaji wa sukari Kenya wanunua miwa kwa bei ya juu

  (GMT+08:00) 2017-08-11 18:11:58

  Wazalishaji wa sukari nchini Kenya wamelazimika kununua miwa kutoka kwa wakulima kwa bei ya juu kinyume na iliyowekwa na kamati ya kuthibiti bei ya miwa nchini humo.Kwa mujibu wa kamati ya kuthibiti bei ya miwa nchini Kenya SCPC, tani moja ya bei ya miwa inatakiwa kuuzwa kwa shilingi elfu 4050 kutoka shilingi elfu 4320. SCPC imesema hatua hiyo inalenga kupunguza bei ya sukari ambayo imekuwa ikipanda na kuwafanya wakenya wengi kushindwa kumudu.Bei hiyo ilishukishwa mwenzi Agosti na kamati hiyo.Maeneo yanayojulikana kwa ukuzaji wa miwa yameshuhudia upungufu wa zao hilo kufuatia ukame ambao umekuwa ukishuhudiwa katika maeneo yao.Mamlaka ya sukari nchini Kenya imesema kuna upungufu wa tani milioni 1.9 wa bidhaa hiyo nchini Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako