• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri wa Viwanda Tanzania afanya ziara ya kushtukiza katika viwanda vilivyobinafsishwa

  (GMT+08:00) 2017-08-11 18:12:30

  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa Tanzania Bw. Charles Mwijage amefanya ziara ya kushtukiza katika viwanda vilivyobinafsishwa na serikali kwa wawekezaji mkoani Morogoro.

  Ziara hiyo aliifanya katika kiwanda cha Moproco, ambako alieleza kufurahishwa na kasi ya utendaji wake huku akiahidi kutoa taarifa rasmi kwa viwanda vilivyokiuka agizo la serikali la kushindwa kufanya kazi miaka 20 tangu vibinafsishwe. Ziara hiyo inakuja siku chache tu baada ya rais John Pombe Magufuli kueleza masikitiko yake kuhusu kushindwa kutekelezwa kwa maagizo yake ya kuvinyakua viwanda vyote vilivyoshindwa kufanya kazi baada ya kubinafsishwa na serikalini. Kiwanda cha Moproco kimeanza kuajiri wafanyakazi kwa awamu na kutokana na utendaji huo, waziri huyo ameagiza mamlaka za ukaguzi kufika kiwandani hapo ili kushauri taratibu mbalimbali zinazotakiwa kufuatwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako