• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani itachukua njia ya kidiplomasia kutatua suala la peninsula ya Korea

  (GMT+08:00) 2017-08-11 18:33:43

  Waziri wa ulinzi wa Marekani Bw. James Mattis amesema, nchi hiyo itachukua njia ya kidiplomasia kutatua suala la peninsula ya Korea.

  Bw. Mattis amesema, Marekani inataka kupata maendeleo ya kidiplomasia, huku akisisitiza kuwa maafa makubwa yataikumba peninsula hiyo kama vita vikitokea.

  Akizungumzia msimamo wa rais Donald Trump wa Marekani kuhusu Korea Kaskazini, Bw. Mattis amesema kuwa rais huyo anajaribu kutatua suala la peninsula ya Korea kwa njia ya kidiplomasia, na msimamo wake mgumu unamaanisha wasiwasi wake juu ya suala hilo.

  Habari zinasema, rais Trump ameionya Korea Kaskazini isitoe kauli za vitisho dhidi ya Marekani ama sivyo itashambuliwa kwa mizinga. Korea Kaskazini imejibu kauli hiyo kwa kusema kuwa inapanga kushambulia kisiwa cha Guam kwa makombora.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako