• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa pendekezo kuhusu hali ya usalama ya Nigeria na DRC

  (GMT+08:00) 2017-08-11 18:34:02

  Naibu balozi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao ameeleza wasiwasi kuhusu hali ya usalama katika nchi za Nigeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, huku akiihimiza jumuiya ya kimataifa kutilia maanani na kuongeza kwa pande zote ulinzi wa makundi yaliyo hatarini wakiwemo wanawake na watoto.

  Bw. Wu amesema hayo katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu amani na usalama wa Afrika. Amesema, DRC na sehemu ya kaskazini mashariki nchini Nigeria zinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mapigano ya kutumia silaha na tishio la kigaidi, hali ya usalama ni mbaya, na wanawake na watoto wa sehemu husika wanakabiliwa na ukatili wa kijinsia.

  Bw. Wu pia amesema, China inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kujenga mazingira ya kimataifa yenye amani, usalama na utulivu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako