• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matokeo ya uchaguzi wa urais wa Kenya yatarajiwa kutolewa leo

  (GMT+08:00) 2017-08-11 18:34:23

  Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya IEBC Bw. Wafula Chebukati amesema, matokeo ya uchaguzi wa urais yanatarajiwa kutolewa leo, huku akiongeza kuwa matokeo ya hesabu ya kura yaliyotangazwa na muungano wa upinzani NASA siyo ya kweli.

  Bw. Chebukati amesema, kisheria, ni tume hiyo tu ndio ina haki ya kuandaa uchaguzi na kutangaza matokeo. Ameongeza kuwa tume hiyo itapata fomu za takwimu za kura kutoka vituo vyote vya upigaji kura kote nchini humo na kutangaza matokeo ya mwisho baada ya kuyathibitisha.

  Habari nyingine zinasema, kaimu waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Bw. Fred Matiang'i amesema, hali ya nchi hiyo ni salama na tulivu, askari wa kutosha wanasubiri amri kupelekwa sehemu yoyote watakayohitajika kote nchini humo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako