• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenyatta achaguliwa rais wa Kenya kwa muhula wa pili

  (GMT+08:00) 2017-08-12 17:20:28

  Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ijumaa ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika nchini Kenya siku ya jumanne iliyopita kwa kupata kura milioni 8.20 sawa na asilimia 54.27 dhidi ya kura milioni 6.76 ambazo ni sawa na asilimia 44.74 kutoka kwa mpinzani wake mkuu Raila Odinga.

  Mwenyekiti wa Tume ya Uhuru na Uchaguzi (IEBC) Wafula Chebukati amemtangaza Uhuru Kenyatta kama rais mteule na William Ruto kama makamu rais mteule na kueleza kuwa tume hiyo ilihakikisha uchaguzi ukifanyika kwa njia huru na ya haki na kuwezesha Kenya kukomaa kidemokrasia.

  Viongozi wa kitaifa wa muungano wa vyama vya upinzani (NASA) wamesema kuwa tume ya uchaguzi imepuuza malalamiko yao na pia wameacha kutoa ombi la kupinga matokeo hayo katika mahakama kuu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako