• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Mataifa waisifu China kwa kuisaidia Cameroon kutatua suala la wakimbizi

  (GMT+08:00) 2017-08-12 17:41:29

  Mkurugenzi wa ofisi ya Shirika la Mpango wa Chakula Duniani la Umoja wa Mataifa WFP nchini Cameroon Bw. Abdoulaye Balde ameisifu China kwa kutoa msaada kwa wakimbizi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati nchini Cameroon, na amesema China imetoa mchango mkubwa katika utatuzi wa suala la wakimbizi la kikanda.

  Kwenye hafla ya kukabidhi msaada wa China iliyofanyika mjini Yaunde, Cameroon, Bw. Balde amesema nchi za Afrika ikiwemo Cameroon zinapopokea misaada ya dharura kutoka China, zinaweza kujifunza uzoefu wa maendeleo ya China.

  Balozi wa China nchini Cameroon Bw. Wei wenhua amesema China ikiwa ni nchi kubwa zaidi zinazoendelea, inatilia mkazo suala la wakimbizi, na siku zote inafanya juhudi kutatua suala hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako