• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu 50 wahofiwa kufa baada ya mabasi mawili kusombwa na udongo kaskazini mwa India

  (GMT+08:00) 2017-08-13 16:12:11

  Watu 50 wanahofiwa kufa baada ya mabasi mawili kusombwa kutokana na udongo kaskazini mwa India katika jimbo la Himachal Pradesh mapema leo.

  Waziri wa usafiri wa jimbo hilo G.S Bali amesema tukio hilo limetokea wakati mabasi hayo yalipokuwa kwenye njia ya kwenda wilaya ya Chamba kutoka mji wa mapumziko wa Manali, na lingine lilikuwa likienda Katra jirani na jimbo la Jammu na Kashmir kutoka Manali.

  Naye naibu kamishna wa jimbo la Mandi Sandiep Kadam, amesema kikosi cha kitaifa cha kukabiliana na maafa kimeitwa kusaidiana na polisi wa huko katika shughuli za uokoaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako