• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tukio la kimabavu lasababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 34 kujeruhiwa huko Virginia, Marekani

  (GMT+08:00) 2017-08-13 16:29:42

  Tukio la kimabavu limetokea kwenye mkutano wa hadharani mjini Charlottesville, jimbo la Virginia, Marekani, na kusababisha kifo cha mtu mmoja, na wengine 34 kujeruhiwa.

  Kabla ya hapo serikali iliamua kuondoa sanamu ya jenerali Robert Edward Lee wa upande wa kusini kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Marekani iliyoko katikati ya mji huo. Tarehe 11 usiku maelfu ya wazalendo walianza kuandamana mjini humo wakidai kwamba wazungu wanapoteza hadhi muhimu nchini Marekani, na kuwataka wazungu kushikamana kupinga watu wa makabila mengine.

  jana mapambano yalitokea kati ya waandamanaji hao na wapinzani wao, na kusababisha watu 15 kujeruhiwa. Siku hiyo mchana, gari moja liliwagonga waandamanaji, na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 19 kujeruhiwa. Idara ya polisi imesema imemkamata mtu aliyeendesha gari hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako