• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa asisitiza kutatua msukosuko wa kibinadamu nchini Yemen kwa njia ya kisiasa

  (GMT+08:00) 2017-08-13 16:30:04

  Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia suala la Yemen Bw. Ismail Ould Cheikh Ahmed amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Mohammad Javad Zarif mjini Tehran. Pande mbili zimekubali kwamba ni muhimu sana kutatua msukosuko wa kibinadamu nchini Yemen kwa njia ya kisiasa.

  Hii ni mara ya pili kwa mjumbe huyo kufanya ziara nchini Iran kwa suala la Yemen. Pia atafanya mazungumzo na naibu waziri wa mambo ya nje wa Iran anayeshughulikia mambo ya nchi za kiarabu na Afrika Bw. Hossein Jaberi Ansari.

  Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani, kuanzia mwezi Aprili mwaka huu, watu zaidi ya 2000 wamefariki kutokana na ugonjwa wa kipindupindu nchini Yemen.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako