• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Katibu mkuu wa UN akitaka chama cha upinzani cha Kenya kitatue mgogoro wa uchaguzi wa urais kwa njia halali

  (GMT+08:00) 2017-08-13 16:33:57

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana amewataka viongozi husika wa siasa nchini Kenya watatue mgogoro wa uchaguzi wa urais kwa njia halali, pia amewahimiza watoe wito wa kutotumia nguvu ya kimabavu kwa wafuasi wao.

  Bw. Guterres siku hiyo ametoa taarifa kwa kupitia msemaji wake, akisema amesikia matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Kenya.

  Bw. Guterres amesisitiza umuhimu wa kuondoa hali ya wasiwasi kwa njia ya mazungumzo. Amesema Umoja wa Mataifa utashirikiana na Umoja wa Afrika, kukutana na viongozi wa Kenya na pande husika mbalimbali, ili kuhimiza mchakato wa uchaguzi mkuu kumalizika nchini humo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako