• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirikisho la Kandanda la Tanzania TFF yapata rais mpya

    (GMT+08:00) 2017-08-14 10:37:50

    Aliyekuwa makamu wa Rais na kaimu wa Rais wa TFF Wallace Karia ametangazwa rasmi kuwa Rais mpya wa TFF kwa kupata jumla ya kura 95 na kuwashida Ally Mayay, Emmanuel Kimbe, Shija Richard, Iman Madegana Fredrick Mwakalebela.

    Kwa ushindi huo sasa rasmi Wallace Karia atatawala nafasi ya Rais wa TFF hadi 2021 makamu wake akiwa ni Michael Richard Wambura aliyewashinda wagombea wenzake wengine watano.

    Punde baada ya kutangazwa mshindi, Karia alisema mchezo wa soka unapendwa na watu wengi lakini kutokana na ubadhirifu, wadhamini wanakimbia, na sasa yeye lengo lake kubwa ni kurejesha hadhi ya soka.

    Karia anachukua nafasi ya Jamali Malinzi, aliye enguliwa kwenye uchaguzi huo kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha za TFF, yeye na Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako